Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwasili kwenye
ukumbi wa Martin's Crosswinds uliopo Greenbelt, Maryland kwenye usiku wa
Wanawake wa Tanzania ulioratibiwa na kikundi cha wakinamama wa tano
chenye maskani yao DMV kinachobeba jina la Tano ladies na kuufanya usiku
huo kuwa wa aina yake na kuweka historia ya wanawake nchini Marekani
kwa kusahau tofauti zao, kuwaacha wapendwa wao nyumbani na kuwa kitu
kimoja kwa kujumuika pamoja kuelimishana juu ya kupendana na kuungana
mkono kila mwenzao anapofanya jambo jema.
Meza alioyokaa Mhe. Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu
wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka akijumuika kwenye usiku wa
wanawake wa Tanzania uliofanyika siku ya Jumamosi June 14, 2014,
Greenbelt, Maryland.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula akiongea machache kwenye usiku huo na
kusisitiza upendo, ushirikiano na mshikamano kwa akina mama na
kuwashukuru tano ladies kwa kuja na mawazo ya kuunda kikundi chao kwa
lengo la kuwaunganisha wanawake wa Marekani na baadae aliwatunukia
zawadi toka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Haika
Lawere ambaye ni mkurugenzi na mmiliki wa Mbezi Garden Hotel Ltd
Tanzania mpenda maendeleo ya akina mama akiongea na kuwaelemisha akina
mama juu ya kupendana na kutokuwa na choyo ya kunyimana fulsa za
maendeleo na kuwasihi wanawake waache raho za kwanini daima tuwe na wivu
wa maendeleo sio wivu wa kurudishana nyuma.
Miriam
Kinunda mwandishi wa kitabu cha Taste of Tanzania akielezea sababu za
yeye kuandika kitabu chake kwa lugha ya kiingereza kwa kusema sababu
kubwa ilikuwa ni kujulisha ulimwengu juu ya mapishi ya Tanzania na kwa
kuwa nipo nje ya Tanzania na lengo ya kitabu changu ilikuwa kukiuzwa nje
ya Tanzania na akatoa mfano wa Mapishi ya China kama yangekua
yanaandikwa Kichina hadhani kama Dunia ingekua inajua mapishi ya Fried
Rice.
Juu na chini Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwazawadia Tano Ladies
Mwenyekiti wa Tano Ladies Asha Hariz akitoa shukurani kwa wanawake wote na kuwashukuru kuwaunga mkono na kukubali wanachofanya.
Asha Nyang;anyi mmoja wa Tano Ladies akiwashukuru wadhamini.
Tano Ladies katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi
No comments:
Post a Comment