UJASIRIAMALI : MHE. PINDA AHUDHURIA MKUTANO WA 5 WA BENKI YA DUNIA, JIJINI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 25 June 2014

UJASIRIAMALI : MHE. PINDA AHUDHURIA MKUTANO WA 5 WA BENKI YA DUNIA, JIJINI DAR ES SALAAM

 
Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari  nje ya Hotel ya Serena ambapo alihudhuria Mkutano wa Tano unaohusu masuala ya Uchumi,kulia kwake ni mkurugenzi wa benki ya Dunia nchini Ndugu Philippe Dongier

 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo aliwaeleza waandishi hao Tanzania ina nafasi kubwa ya kupanua wigo wa ajira kwa kutengeneza mazingira ya kufanyia kazi yenye ubora hasa kwenye  miji inayokuwa kwa kasi hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana na Wanawake.
 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo alikiri pamoja na kukua kwa uchumi lakini bado uchumi haujafungua au kutengeneza ajira kwa wananchi .


Na Benedict Liwenga-MAELEZO. 
WAZIRI Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema kuwa wakati umefika wajasiriamali nchini wanaoendesha shughuli zao katika sekta isiyo rasmi kuboresha shughuli zao ili waweze kuzirasimisha kwa ajili kuboresha maisha yao na Taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Pinda amesema hayo jana (leo) jijini Dar es salaam wakati wa Uzinduzi wa taarifa ya Hali ya Uchumi wa Tanzania-Toleo la Tano iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Dunia.

Taarifa hiyo inalenga kutoa Sera na hatua za kuchukua kuwezesha kupanuka kwa biashara katika miji na majiji nchini kwa ajili ya kuongeza ajira zaidi kwa wananchi na hasa vijana. 




Aidha, Mheshimiwa Pinda alitoa wito kwa vijana nchini kujiajiri katika sekta mbalimbali kama vile kilimo na kukiendesha katika mfumo ulio rasmi ili kiweze kuwakomboa katika maisha yao na kuwasaidia kupata ajira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi na Uganda Bwana Philip Dongier ametoa wito kwa watunga Sera nchini kuweka msisitizo katika kuendeleza ukuaji wa viwanda ili kutengeneza idadi kubwa ya ajira mpya na zenye tija kwa wananchi.

Bwana Dongier aliongeongeza kuwa changamoto nyingi zinazowakabili wajasiriamali wadogo katika kusaka ajira ni fursa zinazotokana na mchakato wa kupanuka kwa haraka kwa miji huku makisio ya hivi karibuni yakionesha kwamba ifikapo mwaka 2030 watanzania wengi watakuwa wakiishi mijini kuliko vijijini.

Taarifa ya Hali ya Uchumi ambayo huchapishwa mara mbili kwa mwaka na Benki ya Dunia inaeleza kwamba kuna uwezekano wa uchumi wa Tanzania kuendelea kukua asilimia 7 kwa mwaka. 

No comments:

Post a Comment