Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa
kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa mwanaume aliyetaka kufunga naye
ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni
habari za kutungwa na hazikuwa na ukweli wowote.
vicky
Vicky ameiambia amplifaya ya Clouds fm jana kuwa maneno mengi ambayo
yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofungwa yalikuwa
yametengenezwa na watu.
“Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja na
hayo mimi bado nasema mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa hajaruhusu kuwa
tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa.
“Mimi kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga
vinginevyo , kwaiyo siku zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo
mapenzi ya binadamu.
“Ni kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba
waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka
2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo
bila kuwa nimemchunguza huyo mtu.
“Kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke wake , mke wake alikwenda kuzuia
Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo
yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest zao ,lakini siyo kwamba
nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu hata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa
kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu aliongea na vyombo vya habari
akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi.
“Kwaiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke wake amezuia yalikuwa ni
maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo kweli.
“Kuhusu kwamba hajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi nafahamu
kwamba yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama ambavyo
mimi naendelea na shughuli zangu kama kawaida, tunawasiliana, yani cha
kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi.
“Hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini mungu
ndo mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwaiyo kama
Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na binadamu
mwingine hataki bado ingefungwa…
“Kwaiyo mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge
wenzangu wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi
ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyo” Alisema
Vicky
No comments:
Post a Comment