AJALI: AJALI MBAYA YATOKEA KATIKA DARAJA LA MTO NDURUMA, JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 20 June 2014

AJALI: AJALI MBAYA YATOKEA KATIKA DARAJA LA MTO NDURUMA, JIJINI ARUSHA


Ajali mbaya imetokea Jana jioni kwa kuhusisha magari matatu katika daraja la mto Nduruma, ambapo gari aina ya Fuso lenye namba T513 BHW lililokuwa likitokea Moshi huku limesheheni machungwa kuyapeleka Arusha limegongana uso kwa uso na Scania Mbili.Hakuna aliyepoteza maisha lakini majeruhi wameumia vibaya.
Eneo la mto Nduruma liliwahi kuongoza kwa ajali hadi kulazimu kuweka matuta makubwa.

Pia ajali hii ilisababisha usumbufu mkubwa wa magari yanayotoka mikoani kuingia na kutoka katika jiji la Arusha. Magari mengine yalilazimika kupitia njia ya Old- Moshi Road inayopitia Moshono hadi Mjini Arusha, na kutokea Usa-River kulekea Moshi na mikoa mingine.

Fuso lililokuwa limebeba Machungwa lilivyoumia

Lori aina ya fuso lilivyoharibika upande wa kulia

Scania mbili zilizogongana na fuso katika daraja la mto Nduruma

Watu wakishangaa ajali ilivyotokea

Machungwa yaliyomwagika katika eneo la daraja ya mto Nduruma Jana.(Picha na Emmanuel Arem)


No comments:

Post a Comment