Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa
na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi
Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa Redio.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa
Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha
mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye akichangia mada.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Picha
juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano
la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari
Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
Mwanakamati wa maandilizi ya
maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014,
Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC),
akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari na
wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano
la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari
Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari
nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na
kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda aliyasema hayo
jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya
maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza
kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na
kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili
unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi ya wahariri
huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa
uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu
moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza kwa kusema
kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na
kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa
kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea
kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii.
Afisa Mipango Kitengo cha
Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha
mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora,
kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari
lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.
“Kwa sasa tasnia hii
iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano
Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai
kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli
hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina
uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.
Kibanda aliongeza kuwa
wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri
zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo
yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa
kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake
mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza
la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa
katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi
katika kuzikabili changamoto zilizopo.
“Kuwe na mtandao
unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili
kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri
kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.
Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada
kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa
kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama
sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani
yanayofikia kilele leo jijini Arusha.
Mwanahabari mwingine
mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya Maadili ya Uandishi wa
Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi kuzingatia uhuru wa habari
walionao kwa kuzingatia maadili yanayowaongoza ili kuboresha heshima
waliyonayo katika jamii kwa kuandika ukweli na uhakika, bila upendeleo,
kutoa fursa ya kujitetea na kukubali kuomba radhi pale unapokosea.
“Kuandika habari zenye
kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko, mashauri na kuongeza
heshima ya chombo cha habari na mwanahabari mwenyewe,”
Akizungumzia suala la
ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari, Kenneth Simbaya,
aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli katika kazi zao na kuacha
kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo litakawaweka huru zaidi katika
utekelezaji wa shughuli zao za uandishi wa habari.
Maadhimisho hayo
yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya uenyekiti wa MISA
TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa kuzindua majarida
mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na kuhitimishwa kwa tafrija
ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mheshimiwa Mark
Bomani.
Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo
Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili
ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa
kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini
Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon
Berege.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
(TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku
moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014
lililofanyika jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni baadhi ya
waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na wanahabari washiriki katika
kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya
Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw.
Fredrick Katulanda, akielezea madhila mbalimbali yaliyomsibu katika
utekelezaji wake wa kuandika habari za uchambuzi.
Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila
Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika
Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la
siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani
2014 lililofanyika jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment