Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova
akionesha sehemu ya vipande 8 vya meno ya tembo vilivyodakwa huko
Tabata Kisiwani jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova akikagua gari linalotuhumiwa kutumika
Sehemu ya mali zilizokamatwa
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata vipande zaidi ya ishirini
(20) vinavyodhaniwa kuwa ni meno ya Tembo vilivyokuwa vimehifadhiwa
nadni ya mfuko maarufu kwa jina la kiroba.
Tukio
hili lilitokea tarehe 30/04/2014 katika kiwanda cha Nondo Steel Master
kilichopo eneo la Mbozi Road (W) kipolisi Chang’ombe (M) kipolisi Temeke
baada ya Polisi kupokea taarifa kuwa katika kiwanda hicho kuna mfuko wa
kiroba wenye bidhaa hiyo umefichwa.
Baada ya taarifa hizo askari kikosi cha Upelelezi walifika kiwandani hapo na kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho aitwaye HITESH S/O PATEL walifanya upekuzi.
Baada ya taarifa hizo askari kikosi cha Upelelezi walifika kiwandani hapo na kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho aitwaye HITESH S/O PATEL walifanya upekuzi.
Katika
upekuzi huo polisi walifanikiwa kukamata vipande 25 vya meno
yadhaniwayo kuwa ni ya KIBOKO vikiwa vimehifadhiwa ndani ya mfuko wa
kiroba ukiwa umefichwa kwenye Roll ambayo ni Malighafi maalum ya
kutengenezea nondo.
Kwa
mujibu wa taarifa ya maafisa wa wanyamapori ni kwamba kwa idadi ya
vipande hivyo 25 ni sawa na VIBOKO 6 waliouawa ambapo meno ya Kiboko
mmoja yana thamani ya Dolla za Kimarekani 1500 sawa na Shilingi za
Kitanzania zaidi ya (Millioni Mbili Laki Nne na Sabini na Tano)
Tshs.2,475,000.
Hivyo
kwa idadi ya VOBOKO sita thamani yake ni sawa na shilingi za kitanzania
THS; 14,850,000/= (million kumi na nne, mia nane na hamsini elfu tu).
Katika
tukio hilo, polisi inawashikilia watu wawili ambao ni RASHID S/O
ABDALLAH, Miaka 19, mwingine ni HEMED S/O JUMA @ KASIMU, Miaka 25.
Washitakiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalowakabili
pindi upelelezi utakapokamilika.
Aidha
katika tukio lingine mnamo tarehe 5/5/2014 huko maeneo ya Tabata
Kisiwani karibu na uwanja wa Twiga Mkoa wa Kipolisi Ilala, Polisi
wamefanikiwa kumkamata MUSA S/O LUCAS KIFARU akiwa naa vipande 8 vya
meno ya tembo vyenye uzito wa kilogram 13.5 ambavyo thamani yake
T.Shs.49,500,000/= vikiwa vimehifadhiwa kwenye begi lenye rangi ya blue
na nyeusi. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa .
No comments:
Post a Comment