Press
Release
Two
years Anniversary of Illegal Elections held in Morogoro May 20th,
2012 under supervision of Leonard Thadeo and National Sports Council of
Tanzania; ‘It’s a shameful act’
May 20th, 2012 RT walifanya uchaguzi kwa MOU
ambapo walisaini kwamba baada ya siku tisini viongozi watakuwa na katiba mpya
ama sivyo watakuwa wamevunja mapatano, August 20th, 2012 siku tisini
zilitimia.
Leo tarehe 20th 2014 ni miaka miwili kamili imepita bila katiba mpya
wala mafanikio yoyote katika mchezo wa riadha zaidi ya aibu kwa taifa letu.
Inaelezwa kwamba mwaka mzima umetimia bila
kikao cha kamati ya utendaji kufanyika kama ilivyo sheria, kanuni na taratibu
za lazima za BMT.
Leo
hii RT imeburuzwa mahakamani (TEMEKE) kwa kudaiwa zaidi ya TSH:
20,000,000 kwa sababu ya uzembe wa viongozi wa taasisi hiyo isiyo na katiba
inayotambulika.
Mapema mwezi huu timu za kwenda kambini nje ya nchi zilichaguliwa mezani badala
ya kuchaguliwa viwanjani kwa vigezo vya kushindanishwa ili walio bora
wapelekwe.
Mbaya
zaidi timu iliyokwenda New Zealand imeripotiwa
kubadilishwa majina kinyemela na kuonekana waliotajwa kuondoka
(Mwa.Samwel Tupa na mwanariadha Atson Mbuga) wapo Arusha na Tanga. Je
nani kaneda? Je posho yao kala nani?
Mheshimiwa
waziri hata kwa macho tu hayo yanayofanywa na viongozi wa RT huyaoni,
pia waheshimiwa wa BMT kimya chenu kinampatia nani tija?
Mkurugenzi
wa Michezo (LEONARD THADEO) ndiye mvunjaji mkubwa wa sheria, kanuni na
taratibu kwani yeye ndiye anayewakingia kifua viongozi haramu wa RT pia ni yeye
alisimamia uchaguzi wa MOU.
Baada ya hayo yote kutokea; Je Anthony Mtaka na nduguye wa ukoo Suleiman Nyambui bado wana uadilifu
usiotiliwa shaka kuendelea kuongoza RT?
Kwa mtindo huu wa kupenyeza wasiohusika katika
safari haiwezi kutumiwa na vikundi hatari kama Al Shaabab na wauza unga?
Arranged and written by:
Wilhelm Francis Gidabuday.
0786778421 / 0752778422.
No comments:
Post a Comment