MCHEZA FILAMU AFARIKI DUNIA : MCHEZA FILAMU WA BONGO MOVIE BW. ADAM PHILIP KUAMBIANA AFARIKI DUNIA LEO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 17 May 2014

MCHEZA FILAMU AFARIKI DUNIA : MCHEZA FILAMU WA BONGO MOVIE BW. ADAM PHILIP KUAMBIANA AFARIKI DUNIA LEO


Adam Kuambiana enzi za uhai wake.
MWIGIZAJI na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo. Marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar. Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo.
Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukitolewa nje ya Hospitali  ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa leo mchana huu.
...Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukiwekwa kwenye gari tayari kupelekwa Muhimbili kuhifadhiwa.
Hospitali  ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam alikofia Msanii Kuambiana.
...Msanii aliekuwa akicheza filamu moja na marehemu katika Hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar akilia kwa uchungu nje ya Hospitali ya Mama Ngoma leo mchana huu.
...Wasanii wakilia kwa uchungu nje ya Hospitali ya Mama Ngoma leo mchana huu.(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)
BLOGU YA WAZALENDO 25 BLOG  IMESIKITISHWA SANA NA KIFO HIKI CHA GHAFLA , MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA.

No comments:

Post a Comment