Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy
akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye
shule hiyo tarehe 10.5.2014.
Mke wa
Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera
akisalimiana na baadhi ya walimu wa Shule hiyo mara alipowasili shuleni
hapo kwa ziara ya siku moja tarehe 10.5.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi (kulia) na wageni wengine wakitembelea
maeneo mbalimbali ya shule hiyo.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akifuatilia jaribio la somo la Fizikia (Hooke’s
Law: Inayosema ‘The force needed to extend or compress a spring by some
distance is proportional to that distance’) lililokuwa likifanywa na
mwanafunzi Mwajuma Mwanankuta wa Kidato cha 4 katika Shule ya Sekondari
ya wasichana ya Mandera tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ya saluti ya Girl Guides kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Mandera .
Mkuu
wa Shule ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy akimkabidhi risala
Mlezi wa Shule hiyo Mama Salma Kikwete alipotembelea shuleni hapo tarehe
10.5.2014.
Mke wa
Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko
wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani Mama Salma Kikwete akizungumza na
wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
shule tarehe 10.5.2014.
No comments:
Post a Comment