MICHEZO NI AFYA : USAJILI WA NAMBA ZA WASHIRIKI UMEANZA RASMI "SOKOINE MINI MARATHON 2014" UNAKARIBISHWA. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 2 April 2014

MICHEZO NI AFYA : USAJILI WA NAMBA ZA WASHIRIKI UMEANZA RASMI "SOKOINE MINI MARATHON 2014" UNAKARIBISHWA.

Namba zimeanza kutolewa kwa washiriki wa mbio za Sokoine Mini Marathon Km 21 na Km 2 ambazo zitatimua vumbi Aprili 12, 2014 Monduli mkoani Arusha, rais Jakaya Kikwete ndiye atakayepuliza kipenga cha kuanza mbio hizo.

Ada ya namba ni Tsh: 2,000 tu, namba zinapatikana Arusha pale Uwanja wa kumbukumbu ya SHEIKH AMRI ABED KARUME na Monduli pia.

Kwa washiriki wote nje ya mkoa wa Arusha wasiliana na VICTOR MACHOTA kwa 0787 415 864 ambaye atapokea usajili kwa njia ya simu na namba yako utajulishwa kwa SMS na itahifadhiwa hadi utakapoichukua. Mwisho wa kuchukua namba yako ni Ijumaa April 11, 2014 Arusha mjini.

Kwa wale watakaosajili kwa njia ya simu tunaomba mtume hela kwa AIRTEL MANEY kwa namba ya Victor Machota, unaombwa uongezee gharama kidogo ya kutoa pesa mtandaoni.

Kwa wale watakaosajili namba papo kwa papo wawasiliane na PHAUSTIN BAHA 0753 860 668 kwa maelezo zaidi na kwa wale wa Monduli wawasiliane na ROBERT MOLEL kwa 0753 739 128.

Kwa ratiba kamili hapo baadae pitia blogu zifuatazo; WOTE MNAKARIBISHWA KUSHIRIKI NA RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA.

-          www.wazalendo25.blogspot.com
 
-          www.victormachota.blogspot.com
 
-          www.gidabuday.blogspot.com

No comments:

Post a Comment