MAADHIMISHO YA SOKOINE NI KESHO: MBUNGE WA MONDULI MHE. EDWARD LOWASSA AKAGUA MAANDALIZI YA SOKOINE DAY, MONDULI JUU, ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 11 April 2014

MAADHIMISHO YA SOKOINE NI KESHO: MBUNGE WA MONDULI MHE. EDWARD LOWASSA AKAGUA MAANDALIZI YA SOKOINE DAY, MONDULI JUU, ARUSHA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa watoto wa Marehemu Edward Sokoine aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Namelok Sokoine (MB) na Joseph Sokoine ambaye ni Afisa katika Ubalozi wa Tanzania nchini Canada, kuhusiana na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli,Marehemu Edward Moringe Sokoine, yatakayoadhimishwa kesho April 12. Rais Jakaya Kikwete ataongoza maadhimisho hayo pamoja na marais na mawaziri wakuu wastaafu.
Kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli,Marehemu Edward Moringe Sokoine.

No comments:

Post a Comment