Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kundi la Wabunge
wa vyama mbalimbali vya siasa walio
marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party
Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo
walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya
ya Madola katika jengo la Durbur jijini London
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aipata picha ya
kumbukumbu na baadhi ya Wabunge wa vyama
mbalimbali vya siasa vya Uingereza walio marafiki wa Tanzania pamoja na
wanachama wa Britain and Tanzania
Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania
Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya
Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu kuendesha mfano
wa mtambo wa kufundishia namna ya kuchimba mafuta katika visima vilivyo bahari
kuu (KCA Deutag Dart Drilling Simulator and Well Enginering System)
alipotembelea Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne
April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini
Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya
Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka huu, ambapo
watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi. Nyuma yake ni ujumbe alioongozana nao ikiwa ni pamoja na Waziri
wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui (kulia) na Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Mhongo (wa pili kulia) Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya
katika Wizara za mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Balozi Dorah Msechu.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ana ujumbe wake katika
picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen,
Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya
kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David
Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho
mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.
No comments:
Post a Comment