wananchi wawakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea jana jioni katika eneo la kia ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruhiwa
Basi aina ya Urio Safaris yenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake moshi kuelekea leguruki mkoani Arusha jana limepinduka katika eneo la kia na kujeruhi watu zaidi ya 31
kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka barabarani
"dereva huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuama barabara ndipo ilipo anguka ghafla na kupinduka mara tatu, hapa unavyoiona tumeigeuza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina
mpaka kamera ya Wazalendo 25 Blog inaondoka eneo la tukio watu 31 walikuwa wamekwisha pelekwa katika hospitali ya wilaya ya hai kwa ajili ya matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya leguruki ambao walikuwa wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya pasaka .
picha ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye basi hilo aina ya Urio Safaris lililopata ajali jana jioni katika eneo la Kia wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
Picha na Woinde Shizza wa blogu ya Wazalendo 25 Blog |
No comments:
Post a Comment