FILAMU NA USAFI WA MAZINGIRA : WASANII WA FILAMU TANZANIA WAMUUNGA MKONO ROSE NDAUKA KATIKA KAMPENI ZA KUSAFISHA JIJI LA ILALA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 18 March 2014

FILAMU NA USAFI WA MAZINGIRA : WASANII WA FILAMU TANZANIA WAMUUNGA MKONO ROSE NDAUKA KATIKA KAMPENI ZA KUSAFISHA JIJI LA ILALA



Kutokana na Takwimu iliotolewa miezi kadha iliopita kuhusu Tanzania kuwa nchi chafu huku, Dar es salaam ndo ukiwa mji uliotolewa macho kwa kuwa na uchafu mwingi sana, Kupitia kampuni yake ya Ndauka Entertainment Muigizaji Rose Ndauka ameamua kuhamasisha wananchi wa Kitanzania kuweka mazingira safi, akishirikiana na baadhi ya wasanii aliowaalika kusaidiana nae kwenye kuhamasisha wananchi kupitia Kampeni yake ya NG'ARISHA TANZANIA, Kampeni hii ilihusisha kuhusu kufagia baadhi ya mitaa katika manispaa ya ilala, kuzoa taka na kuzitupa maeneo husika au kuziteketeza huku akishirikiana na kampuni ya Green Waste Disposal.


' Huu ni mwanzo tu, tutaendelea tena, nafanya hivi kuwastua watanzania wezangu kwa jinsi gani tulivyojisahau kwenye mazingira kwani hii inaleta sifa mbaya"alisema Rose ndauka



Wafanyakazi wa Waste Disposal wakishiriki kwenye kampeni hio

Baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi waliojitokeza
Rose Ndauka akifanya mahojiano na waandishi waliojitokeza
Baada ya wasanii pamoja na baadhi ya wadau

Msanii Yvonne akihojiwa na Muandishi wa Channel Ten Clement Silla

No comments:

Post a Comment