URAFIKI KIMATAIFA :KAMISHNA WA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA ATEMBELEA MAGEREZA TANZANIA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Feb 2014

URAFIKI KIMATAIFA :KAMISHNA WA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA ATEMBELEA MAGEREZA TANZANIA

PIX 1 
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (wa nne kulia) akiwa na  Jenerali wa Magereza Tanzania John Minja (katikati)  wakimsiliza kwa makini Mnadhimu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mmeta Manyara akijitambulisha. Kamishna Chato  ametembelea Makao Makuu ya Magereza ikiwa kni ziara ya siku sita nchini Tanzania.Wa tatu kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Yumbe, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Tebuho Nyambe na wa kwanza ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza James Nkoloma wote kutoka Makao Makuu ya Magereza nchini Zambia. PIX 2Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato ( wa nne kushoto), akipokea taarifa fupi kutoka kwa mmoja wa maofisa  kiwandani Ukonga. Kamishna Percy alitembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga, Dar es salaam kuona shughuliza za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanyika. PIX 3Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato akisaini kitabu cha wageni Kiwandani Ukonga, wa pili kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Tanzania Dkt Juma Ali Malewa.
PIX 4
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (katikati) akifurahia kukaa katika moja ya samani zinazotengenezwa kiwandani Ukonga, kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Tanzania, Dkt Juma Ali Malewa na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza wa Zambia John Yumbe. PIX 6Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato wa (pili kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa mafundi katika Karakana ya magari ya Magereza iliyoko Ukonga Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa.
PIX 7
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akipokea salaam ya heshima kutoka kwa Paredi maalum (halipo pichani) lililoandaliwa maalum kwa jairi yake katika uwanja wa paredi wa Chuo Cha Maafisa wa Magereza Ukonga.Nyuma yake ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa na mwenye nguo za kijani ni Kaimu Mkuu wa Chuo  Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundi.
PIX 8
Kamishna wa Magereza nchini Zambia  Percy Chato (mwenye suti) akikagua paredi maalum lililoandaliwa kwa heshima yake katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Dar es salaam.
PIX 9
Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) cha Ukonga jijini Dar es salaam wakionesha aina mbalimbali za mzoezi ya kujihami na kuanguka bila kuumia katika kukabiliana na hatari yoyote, mblele ya Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (hayupo pichani)
PIX 10
Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (katikati) akifurahia “juice” ya madafu aliyoandaliwa katika viwanja vya Garden Ukonga Dar es salaam wa pili kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Nchini Dkt. Juma Ali Malewa na wa Kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza nchini Zambia John Yumbe kwa pamoja wakifurahia “juice” ya madafu. PIX 11kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Kikosi Maalum cha KMKGM jinsi ya kujiandaa ktuliza ghasia magerezani au popote pale itakapohitajika. Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja wa Magereza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad