MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM :DKT JAKAYA KIKWETE AONGOZA SHEREHE HIZO,WASANII WA FILAMU WAJIUNGA NA CCM - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Feb 2014

MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM :DKT JAKAYA KIKWETE AONGOZA SHEREHE HIZO,WASANII WA FILAMU WAJIUNGA NA CCM

 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali Rashid Mkwinda , Bashir Nkoromo na wengine wakishiriki kuchukua matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
 
Rais Kikwete akiongoza  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto akiwa sambamba na baadhi ya watoto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo. 
 Baadhi ya vijana wakereketwa na chama cha CCM wakiwa na mabango yao. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  (pilia kulia) akiwa tayari kuongoza wanachana na Wananchi (hawapo pichani) kushiriki matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Bwa.Phillip Mangula,wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji pamoja na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya wakiwa tayai kuyaanza matembezi hayo.
 Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya watoto waliokuwa miongoni mwa watoto waliojitokeza kushiriki  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema  asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad