Balozi
wa Tanzania Nchini Marekani na Canada Balozi Liberata Mula mula
akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kwa mazungumzo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi
wa Tanzania Nchini Marekani na Canada Balozi Liberata Mula mula hapo
Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
**********************************
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa kwa hatua iliyochukuwa ya
kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kwa
mafanikio makubwa na ya kupigia mfano.
Pongezi
hizo zimetolewa na Balozi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Nchini Marekani na Canada Balozi Liberata Mulamula wakati
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
hapo Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi
Liberata Mula mula alisema maadhimisho hayo yaliyofikia nusu Karne
yameijengea Historia kubwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika
muelekeo wa maendeleo ya Kiuchumi na Ustawi wa Jamii.
Alisema
Mataifa mbali mbali duniani yameendelea kushuhudia hatua kubwa
zilizofikiwa na Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo akiitaja
baadhi yake imo katika sekta ya Afya, Maji, Mawasiliano ambayo tayari
imeshajengewa miundo mbinu imara.
“
Huu ni mwaka wa Kihistoria kwa Zanzibar na Tanzania katika kuadhimisha
miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964. Sasa
kinachowapaswa wananchi na viongozi wote kuhakikisha historia hii
inaendelezwa zaidi katika misingi ile ile ya amani na utulivu “. Alisema
Balozi Liberata Mula mula.
Balozi
Mula mula alielezea kwamba katika muelekeo wa kujiandaa na sherehe za
maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
Uongozi wa Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani na Canada
tayari uko mbioni kujiandaa na tamasha kubwa litakalolenga kutangaza
maendeleo yaliyofikiwa na Tanzania katika kipindi hicho.
Alisema
Ofisi yake iko wazi na huru wakati wote kujumuisha pamoja na taasisi
mbali mbali ziwe za Serikali au Binafsi katika kuchangia na hatimae
kufanikisha Tamasha hilo muhimu katika kuitangaza Tanzania kiuwekezaji.
Akizungumzia
kuhusu ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mjini
Seattle Nchini Marekani mwishoni mwa Mwaka jana Balozi Liberata Mula
mula alisema yapo mafanikio makubwa yaliyojitokeza kufuatia ziara hiyo
ambayo yanatarajiwa kuinufaisha kiuchumi Zanzibar.
Balozi
Mula mula alisema kilichopo hivi sasa ni kuhakikisha taasisi
zinazohusika na ziara hiyo kuendelea kufuatilia mazungumzo au
makubaliano iliyofikia ili lengo la ziara hiyo liweze kufanikiwa vyema.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Zanzibar ina mategemeo makubwa ya kuongezeka kwa miradi ya
uwekezaji katika sekta ya utalii kutokana na miundo mbinu mbali mbali
iliyowekwa.
Balozi
Seif aliuomba Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani na Canada kuhakikisha
kwamba unaendelea kuitangaza Zanzibar kiuwekezaji ili washirika na
taasisi za maendeleo wapate nafasi ya kuitumia fursa hiyo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza watendaji wote wa Ofisi za
Kibalozi za Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani kwa kufanya kazi
za kizalendo licha ya kukabiliwa na mazingira magumu ya kikazi.
No comments:
Post a Comment