MKUTANO WA VVU : MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU KUTOKOMEZA VVU KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 22 January 2014

MKUTANO WA VVU : MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU KUTOKOMEZA VVU KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid, kwenye hoteli ya Serena alikoenda kufungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kulia) na Mheshimiwa Mama Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, (kushoto), wakielekea kwenye chumba cha mkutano.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto uliofanyika kwenye hoteli ya Serena.
Dr. Khadija Mwamtemi kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, alikuwa ni mmojawapo kati ya washiriki waliochangia mawazo yao mara baada ya mada mbalimbali kutolewa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo pichani). Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam tarehe 21.1.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment