Na Rashid
Nchimbi wa Jeshi la PolisiArusha
Watu saba wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa na misokoto
5000 ya madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja na mirungi kilo 47.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la
Mti mmoja lililopo wilaya ya Monduli.
Mafanikio hayo yalitokana na msako shtukizi uliofanywa na jeshi
la polisi Mkoani hapa kuanziasaa 12:00 asubuhi mpaka saa 10:00
jioni baada ya kufanya upekuzi katika magari mbalimbali nakupata madawa hayo ambayo yalikuwa yanasafirishwa nawatuhumiwa hao kupitia magari ya abiria yaliyokuwa ya kielekea Manyara,
Singida, Dodoma na Mwanza.
Akizungumza na waandishi wahabari ofisi kwake,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Liberatus Sabas watuhumiwa hao walikuwa wanayahifadhi madawa hayo kwenye mifuko ya
“plastic” ili yasitoe harufu nakisha kuweka kwenye mabegi.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Godwina Munisi
(31) Mkazi wa Sombetini , Mwajuma Kingu (48) Mkazi wa Mbauda, Fidelis Joseph (48) Mkazi wa Ngarenaro,
Selemani Ally (34) Mkaziwa Olmatejoo, Omari Ally (25) Mkazi wa Babati Mkoani Manyara Kasimu Ayubu
(39) Mkaziwa Tarakea Rombo Mkoani Kilimanjaro na Yasini Talian (40)
Mkaziwa Ngarenaro.
Kamanda Sabas alisema kwamba watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baadaya upelelezi kukamilika.
Wakatihuohuo katika msako unaoendelea wilayani Longido,jumla ya magunia
16 ya madawa ya kulevya aina ya bangi yamepatikana katika eneo la kijiji cha
Leboo baada ya askari Polisi kufanya msako nakufanikiwa kupata magunia hayo 16
yaliyokuwa yanasafirishwa .
Kamanda Sabas alisema kwamba,
askari hao walikuwa wanafanya msako usiku na mara baada ya watuhumiwa hao kugundua kuwa wanafuatiliwa walitelekeza magunia hayo
16 na kukimbia. Inasemekana kwamba watuhumiwa hao walikuwa wanatumia wanyama aina ya Punda kusafirishia madawa hayo ambapo magunia yalikuwa yamefungwa mawili mawili.
Hata hivyo Jeshi la
Polisi Mkoani hapa bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao iliwafikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.
No comments:
Post a Comment