MAWAZIRI WALAZWA : DKT. GHARIB BILAL AWAJULIA HALI MAWAZIRI WALIOLAZWA MUHIMBILI, CLEOPA MSUYA NA HARUNA ALI SULEIMAN - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 15 January 2014

MAWAZIRI WALAZWA : DKT. GHARIB BILAL AWAJULIA HALI MAWAZIRI WALIOLAZWA MUHIMBILI, CLEOPA MSUYA NA HARUNA ALI SULEIMAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali. Kushoto ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Haruna Ali Suleiman, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali Jan 15, 2014. Katikati ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga. Picha na OMR Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment