Askofu mkuu wa kanisa la Katoliki, jimbo kuu la Arusha Josephat Lobulu akitoa pole kwa baadhi ya majeruhi wa bomu. |
Watu sita wamejeruhiwa na kile kinachodhaniwa ni bom la kurusha eneo la lake tatu Usa-river wilayani Arumeru mkoani Arusha siku ya mkesha wa mwaka mpya walipokuwa wakitoka kanisani kuelekea majumbani kwao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika hospitali ya Tengeru iliyopo wilayani Arumeru, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo walisema kuwa siku ya mkesha wa kuupokea mwaka 2014 walipokuwa wakitoka kanisani (Kanisa katoliki parokia ya USA river) waliweza kusikia mlio mkubwa wa kitu kama bom la kurusha ndipo baadhi yao walioangukiwa na bom hilo kuweza kujeruhiwa vibaya na kuanguka chini huku wakivuja dam nyingi sehem mbalimbali za mwili.
Walisema kuwa bom hilo lililorushwa na Askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha lilikuwa na lengo la kuwatawanya watu waliokuwa wakichoma matairi barabarani katika eneo hil ikiwa kama sehemu ya kusherehekea mwaka 2014.
Kwa upande wake Askofu mkuu wa kanisa la katoliki jimbo kuu la Arusha, Josephat Lebulu akizungumzia tukio hilo alisema kuwa ni tukio la kulaaniwa, hivyo ameliomba jeshi la polisi kushughulikia jambo hilo.
Alisema kuwa amesikitishwa na tukio hilo, lakini yeye kama mtumishi wa Mungu anapaswa kuwaombea wote walioathrika na tukio hil ikizingatiwa wamepatwa na tukio hilo mita chache tu kutoka katika nyumba ya Mungu (Kanisani).
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas. |
"Taarifa nimezipata lakini uchunguzi unaendelea kujua chanzo na muhusika sambamba na ukweli wa mlipuko huo ili kujua kama kweli ni bomu na ni la aina gani". Na Bertha Blog
No comments:
Post a Comment