Na Zamaradi Kawawa
Shirika la Posta Tanzania limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi
Bilioni 44.5 kufikia mwaka 2012 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa
huduma zake hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Posta Masta Mkuu Bw. Deos Mndeme wakati alizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafaniko yaliyofikiwa na shirika hilo tangu kuanzishwa kwake.
Mndeme amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na huduma bora zenye hadhi ya kimataifa zinazotolewa na shirika hilo kwa wananchi hali itakayosaidia kuongeza mapato ya Serikali.
“Shirika limejipanga zaidi kutumia TEHAMA katika kuboresha huduma zake ikiwa ni moja ya mkakati utakaosaidia serikali kuongeza mapato na kufikia malengo ya muda mrefu yaliyowekwa na shirika pia tumejipanga kuendelea kuboresha huduma tunazozitoa ili kuendana na mahitaji ya wakati” alisema Mndeme.
Mndeme aliongeza kuwa kwa sasa shirika limeunganisha Ofisi 86 kwenye Wilaya na Miji kote nchini na mfumo wa mawasiliano ili kuongeza idadi ya wateja wanaohudumiwa,kuondoa ucheleweshaji na kuondoa malalamiko ya wateja.
Katika kuhakikisha shirika linashiriki kikamilifu katika shughuli za kitaifa Mndeme alisema shirika litafanya uzinduzi wa toleo jipya la stempu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe hizo zitakazofanyika Disemba 28 mwaka huu.
Shirika la Posta ni mwanachama wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) ambalo Tanzania ilijiunga mwaka 1963 na kwa hivi sasa idadi ya nchi wanachama wa umoja huo ni 192 malengo ya Umoja huo ni pamoja na kuisimamia,utumiaji wa barua,Vipeto,Vifurushi katika nchi mbalimbali duniani,kutoa ushauri,usuluhishi,kuunganisha ushirikiano baina ya nchi wanachama na kutoa misaada ya kiufundi.

No comments:
Post a Comment