Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Maria Bilia
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya Viwanda Afrika ambapo
alielezea mafanikio na changamoto katika sekta ya viwanda nchini na
Afrika kwa ujumla. Kulia ni Afisa mipango wa Taifa kutoka Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Gerald Runyoro.
Afisa
Mipango wa Taifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya
Viwanda (UNIDO) Bw. Gerald Runyoro akizungumzia ushiriki wa shirika hilo
katika kukuza viwanda nchini.
Kaimu
Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) Dr. Samwel Nyantahe
akizungumzia umuhimu wa kuongeza thamani za bidhaa zinazozalishwa hapa
nchini kwa minajiri ya kupambana na tatizo la ajira.
Mkurugenzi
wa Viwanda vidogo vidogo kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko
Dakta. Consolatha Ishebadi (katikati) akifafanua changamoto wanazokutana
nazo wafanyabiashara wazawa katika kutengeneza vifungashio vyenye ubora
(Packaging) kwenye bidhaa zao.
Mwandishi kutoka gazeti la The Citizen akiuliza swali wakati wa mkutano huo wa siku ya Viwanda Afrika.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.........
Na Damas Makangale, Moblog
SERIKALI
imesema haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara
wote kutoka nje wanaofanya biashara au kufungua viwanda vidogo vidogo
bila kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi. Moblog inaripoti.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika kuadhimisha Siku ya Viwanda Afrika jijini
Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na
Masoko, Bi. Maria Bilia amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara toka nje
ambao hawataki kufuata taratibu za uwekezaji na sheria za nchi.
“Matokeo
ya kutokufuata sheria za nchi katika uwekezaji au ufanyaji wa biashara
ni uanzishwaji wa viwanda vinavyozalisha bidhaa ambazo hazikidhi
viwango na ni hatari kwa Afya za walaji,”
“Sheria
za nchi zipo wazi kwamba lazima Kituo cha Uwekezaji (TIC) na Brela
msajili wa biashara wahusishwe kwenye mchakato mzima wa uwekezaji au
biashara yeyote ndani ya nchi,” Bilia amesema
Amesema
vile vile Wizara ya Viwanda kwa kushirikiana na Wizara zingine na
taasisi za Serikali wanaendelea kurahisisha urasimishaji wa biashara kwa
wanyonge kupitia mradi wa Mkurabita Mkakati wa Kurasimisha Biashara kwa
Wanyonge ili kuwawezesha wazawa kufanya biashara zenye tija kwao na
taifa kwa ujumla.
Bi.
Bilia aliendelea kusema kuwa siku ya viwanda Afrika ilianzishwa mwaka
1989 na Tanzania ilijiunga rasmi mwaka 1990 katika kuhamasisha ukuaji wa
viwanda katika kukuza uchumi wa nchi za Afrika.
Amesema
sekta ya viwanda ikishirikishwa na sekta zingine inaweza kufanya
mabadiliko haraka katika maisha ya mtu mmoja mmoja hususani ajira na
hutoa bidhaa bora kwa matumizi ya binadamu.
Alisisitiza
kuwa mwaka huu Serikali imepanga kuwa na maonyesho ya wiki nzima
yatakayofikia kilele tarehe 20 mwezi huu ambapo wafanyabiashara
mbalimbali watapata fursa ya kuonyesha bidhaa zao katika ukumbi wa PTA
saba saba.
Amesema
kauli mbiu ya mwaka huu ni “ Ni Ajira na ujasiriamali, Fursa ya
Kuharakisha Maendeleo ya Viwanda Afrika katika juhudi za kupunguza
makali ya umaskini na tatizo la ajira kwa vijana.
Kwa
upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI)
Dkt. Samwel Nyantahe amesema shirikisho la viwanda linaunga mkono juhudi
za serikali katika kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa hapa
nchini ili kuongeza mapato ya nchi.
“Sisi
Shirikisho la Viwanda kwa kushirikiana na serikali na watu binafsi
tutaendelea kuhamasisha jamii umuhimu wa viwanda katika kuongeza thamani
ya bidhaa na kupambana na tatizo la ajira nchini,” amesema
Bw.
Gerald Runyoro kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya
Viwanda (UNIDO) amesema umoja wa mataifa kwa kushirikiana na serikali na
wadau wengine wataendelea kusisitiza watu kuwekeza na kufungua viwanda
ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi Afrika.
Amesema
wafanyabiashara lazima wawe na ujasiri wa kufungua biashara au kiwanda
katika juhudi za kuongeza thamani bidhaa zitokazo Afrika na kutafuta
fursa za uwekezaji nje ya Afrika.
No comments:
Post a Comment