Mwenyekiti
wa kamati hiyo Dk.Khamis Kigwangalla katikati na Mbunge wa
Arusha mjini Godbless Lema wakipata maelezo kutoka kwa injinia wa jengo
la hospitali ya Levolosi hivi karibuni
Kamati ikiwa makini kufuatilia mchakato
Meza kuu ndani ya kikao cha kamati
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiangalia nyufa katika jengo la hospitali ya Levolosi akiwa na Mbunge wa Dole Zanzibar Sylvester Mabumba
Na Pamela Mollel, wa JAMII BLOG
Kamati ya Bunge
ya serikali za mitaa (TAMISEMI)inaiagiza serikali kuwasimamisha kazi
watumishi wote waliohusika katika ugawaji wa viwanja( 20) vyenye mgogoro
katika halmashauri ya jiji la Arusha ili kupisha uchunguzi baada ya
kubaini uwepo wa ugawaji usio halali wa viwanja katika maeneo ya wazi
katika kipindi cha mwaka 2000 na 2006.
Kauli hiyo
ilitolewa hivi karibuni jijini hapa na mwenyekiti wa kamati hiyo
Dk.Khamis Kigwangalla wakati akitoa maazimio ya kamati baada ya ziara
yao ya siku nne iliyolenga kukagua miradi mbalimbali na maeneo yenye
mgogoro katika Halmashauri ya jiji la Arusha
Aidha katika
mkutano huo Mwenyekiti wa kamati hiyo alifanya mahojiano ya kina na
wahusika mbele ya kamati na kujiridhisha kuwa kulifanyika ufisadi wa
kutisha katika ugawaji wa viwanja hivyo.
Dk.Kigwangalla
alisema kuwa kamati hiyo inaiagiza serikali kuwachukulia hatua kali za
kisheria kwa watumishi wote waliohusika katika sakata hilo la ugawaji wa
viwanja,ikiwepo kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa kina wa
kamati pamoja na kuwapa maelekezo ya namna ya kuripoti kila siku katika
eneo husika
Katika ziara hiyo
kamati iligundua kuwa nyaraka mbalimbali zinazohusiana na maeneo hayo
kuwa na mapungufu makubwa huku ikipelekea viwanja hivyo kugawiwa
kinyemela kwa wamiliki wa viwanja hivyo.
Pia kamati hiyo
iliazimia kusimamisha vibali vyote vya ujenzi katika maeneo yenye
mgogoro huku Mwenyekiti wa kamati hiyo akitaja maeneo hayo kuwa ni
pamoja na uwanja wa ngarenaro,hospitali ya levolosi,Viwanja vya dampo,na
vingine vyenye mgogoro
.Dk Kigwangalla
wataja wafanyakazi hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa Idara ya
Ardhi, Mrimba Maghembe na wa Mipango Miji, Richard Ndagamasa na msaidizi
wake, Elly Kirenga, pamoja na mtumishi mwingine aliyemtaja kwa jina
moja la Urassa.
Pia katika hali
isiyokuwa ya kawaida, Kamati hiyo imeiagiza serikali kuhakikisha
inawatafuta, Sadic Abdallah Sadic, anayedaiwa kuuziwa viwanja vingi
vyenye mgogoro huku nyaraka zilizo na picha na saini yake zikiwa na
walakini na kutakiwa kufikishwa mbele ya kamati hiyo kutokana na kuitwa
kwa siku tatu na kushindwa kufika.
Akiongelea
kiwanja cha Njiro, alisema kuwa kilitengwa kwa ajili ya ujenzi ya
hospitali, kituo cha polisi na mahakama ya tarafa, ambapo ekari nne
zilikuwa kwa ajili ya kumfidia mwananchi ambaye eneo lake liliuzwa kwa
mtu mwingine.
Alisema kuwa
wakati halmashauri ikiwa kwenye mchakato wa kumnyang’anya mwekezaji huyo
eneo hilo likauzwa kinyemela kwa mfanyabiashara Cicram Jeetu Patel
pamoja na mkewe Sabira, ambao sasa wamebadili jina wanajiita Kampuni ya
Njiro Medical Comple.
No comments:
Post a Comment