TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 17. 10. 2013. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 17 October 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 17. 10. 2013.





WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 16.10.2013 MAJIRA YA SAA 22:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHENJE KATA YA MYOVIZI, TARAFA IYULA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA.  MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA  KIUME, UMRI KATI YA  MIAKA 20-25,  ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA  MWILI WAKE  KUTUPWA KWENYE SHAMBA MALI YA  FRIDAY S/O BUKUKU. CHANZO KINACHUNGUZWA.  MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA JERAHA UBAVU WA KULIA, UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 16.10.2013 MAJIRA YA SAA 02:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISALALO, KATA YA MSIA, TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. TUSAMALE S/O MWILEGA, MIAKA 70, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA ISALALO ALIFARIKI DUNIA AKIWA AMELALA NDANI YA  NYUMBA YAKE  BAADA YA  MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KUCHOMA MOTO NYUMBA YAKE. MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE KATIKA NYUMBA HIYO ILIYOJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA KWA KUTUMIA NYASI.  CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment