Mhe.
Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara
akilakiwa na Afisa Habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi
Kasiga(kulia) wakati alipowasili Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
siku ya Alhamisi Oct 24, 2013 kati ni Katibu wa wizara hiyo mhe. Juma
Mswadiku
Mhe.
Waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara
akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata
Mulamula kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe.
Waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara
akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani, Balozi Watanzania nchini Marekani Mhe. Mulamula na Afisa
Habari wa Ubalozi, Mindi Kasiga wakiangalia.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwaongoza
wageni wake Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara na Katibu wa Wizara hiyo kwenda kukutana na Maafisa wa
Ubalozi kwenye ukumbi wa mikutano wa kumbukumbu ya Mwl. Julius Nyerere.
Mhe.
Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico
akimkaribisha rasmi Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dkt. Fenella Mukangara kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na
kufanya Utamburisho kwa Maafisa Ubalozi kujitamburisha kwa Mhe. Waziri
kwa kutaja majina yao na nafasi zao za kazi kwenye Ubalozi huo.
Maafisa
Ubalozi wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata
Mulamula wakati alipokua akimtamburisha Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara kwenye ukumbi wa mikutano
wa Mwl. Julius Nyerere
Mhe.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akiongea na Maafisa wa Ubalozi akiwapa salamu kutoka Tanzania na
kuwaeleza mambo mbalimbali yanayoikabili nchini yetu yakiwemo swala la
wahamiaji haramu na jinsi gani serikali inavyokabiliana nalo, swala
lingine ni kuhusu ajira kwa Vijana, juhudi anazofanya kuwaelimisha
Vijana jinsi ya kujiajiri wenyewe na pia alizungumuzia sekta binafsi
kama zikifanya vizuri zitasaidia sana maendeleo ya nchi yetu na kutilia
msisitizo swala la michezo mashuleni pia alielezea maswala ya vyombo vya
habari na mchakato wa rasimu ya katiba unavyoendelea hizi sasa
Tanzania. Baada ya maelezo ya Mhe. Waziri kulikuwa na kipindi cha
maswali na majibu na kuchangia hoja mbalimbali kuhusu maendeleo ya
nchini yetu.
Mhe.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula
wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi huo, kutoka kushoto ni
Mwambata wa Jeshi Colonel Adolph Mutta, Afisa Paul Mwafongo, Afisa
Switebert Mkama, Afisa Agnes Lusinde, Afisa Mindi Kasiga, Mhe. Waziri,
Mhe. Balozi aliyesimama nyuma ya Balozi ni Afisa Catherine Kijuu, Mkuu
wa Utawala Mama Lily Munanka, Afisa Suleiman Saleh, Afisa Emmanuel Swere
Alfred na Afisa Abbas Missana.
No comments:
Post a Comment