Mshindi wa kwanza wa mbio za Rock City Marathon 2013 kilomita 21 kwa upande wa wanaume Alphonse Felix kutoka mkoani Arusha akimalizia mbio hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo alitumia saa 1:02:17 na kufanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka jana na Opio Chacha aliyetumia saa 1:05:47. |
Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,500,000/= mshindi wa kwanza mbio za Rock City Marathon kilomita 21kwa upande wa wanaume Alphonse Felix ambaye pia alijinyakulia zawadi ya tiketi ya ndege toka moja wa wadhamini wa mbio hizo Precission Air, ya kuelekea Dar es Salaam na kurudi mkoani kwake Arusha. |
Afisa Mauzo wa King’amuzi cha Continental, Dominic Kiluma akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa Joel Kimbiaye toka Kenya mara baada ya kuibuka mshindi wa nafasi ya pili mbio za Rock City Marathon 2013 ambapo pia mshiriki huyo alijinyakulia kitita cha shilingi 900,000/=. |
Afisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta akikabidhi zawadi ya shilingi 700,000/= mshindi wa tatu katika mbio za Rock City Marathon kilomita 21, Andrew Sambu ambaye pia alijinyakulia king’amuzi cha Continental. |
Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,500,000/= mshindi wa kwanza mbio za Rock City Marathon kilomita 21 kwa upande wa wanawake Vicoty Chepkemoi kutoka Kenya. |
Afisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 900,000/= mshindi wa pili wa mbio za Rock City Marathon kilomita 21 wanawake Sarah Ramadhan ambaye pia alinyakuwa king’amuzi cha Continental. |
Afisa Mauzo wa King’amuzi cha Continental Dominic Kiluma akikabidhi zawadi ya king’amuzi kwa mshindi wa tatu mbio za Rock City Marathon 2013 wanawake, Zakia Mrisho ambaye pia alijinyakulia kiasi cha shilingi 700,000/= |
Washiriki wa Rock City Marathon 2013 wakichuana vikali kuisaka nafasi za ushindi wa mbio hizo ili kujinyakulia zawadi mbalimbali zilizoanishwa na wadhamini wa michuano hiyo ambao iliandaliwa na ampuni ya Capital Plus International Limited kwa kushirikaina na wadhamini mbalimbali. |
Washiriki kutoka Australia wakimaliza mbio za kilomita 21. |
Baadhi ya raia wa nchi za kigeni wakipumzika baada ya kumaliza mbio za Rock City Marathon |
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2, Benedicto Mashauri wa mwanza, baada ya kuwashinda watoto wenzake 284 walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2013 |
Mkurugenzi wa Club ya Holili Youth Athletics iliyoko mkoani Kilimanjaro wilayani Rombo Domian Rwezaura Janand, akitamba mara baada ya mashindano kwa washiriki toka kambi yake kufanya vyema kwenye mbio za Rock City Marathon 2013 |
Sehemu ya watoto waliowakilisha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2013. |
Mbio za Rock City Marathon 2013 zafana
WANARIADHA Alphonce
Felix kutoka Arusha na Vicoty Chepkemoi kutoka Kenya wameibuka vinara
katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 yanayojulikana kama ‘Rock
City Marathon 2013’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili
nakujinyakulia Shilingi milioni moja na nusu (Sh 1.5 m) kila mmoja.
Alphonce alishinda mbio hizo
kwa upande wa wanaume baada ya kutumia saa 1:02:17 hivyo kuvunja rekodi
iliyowekwa mwaka jana na mwanariadha Kopiro Chacha aliyetumia 1:05:00,
huku Chepkemoi aki kutumia 1:12:44.
Nafasi ya pili alishika Joel
Kimtiae wa Kenya kwa upande wa wanaume na Sarah Ramdhani kutoka Arusha
kwa upande wa wanawake, wakifuatiwa na Sambo Andrea kwa upande wa
wanaume na Zakia Mrisho kwa upande wa wanawake wote wakitokea Tanzania.
Zaidi ya wanariadha 1090 walijitokeza kushiriki mashindano hayo
yanayoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International kwa mwaka wa
tano mfululizo.
Wambura Lameck kutoka Holili alingara katika mbio za kilometa tano huku Dotto Ikangaa kutoka Arusha akishika nafasi ya pili .
Kwa mujibu wa waratibu wa mbio hizi, udhamini waliopata kutoka kwa
wadamini ambao ni, Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF), Africa
Barrick Gold (ABG), Precision Air, Airtel kupitia Airtel Money, TANAPA,
Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara
Communications, Continental Decoders na Umoja Switch, umewawezesha
kuboresha tuzo kwa washiriki pamoja na kufanya maadalizi mazuri
yanayozingatia sheria za riadha.
Washiriki na washabiki wa mbio za Rock City za mwaka huu walipata
kuburudishwa na kikundi cha Sanaa cha Bujora ambacho kilionyesha umahiri
wake wa kuonyesha utamaduni wa kitanzania kupitia dansi.
Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw Kizito Bahati (Afisa michezo
Manispaa ya Ilemela), mbali na kutaka washiriki kutoka kanda ya ziwa
kuchangamkia fursa inayoletwa na mbio hizo, pia aliwataka viongozi wa
vyama vya riadha kuwa na program endelevu ya kukuza mchezo wa riadha kwa
kushirikiana na Maafisa Michezo wa Mikoa na Wilaya ili waweze kupata
fursa ya kufikisha na kuufundisha mchezo huu katika shule ambako ndio
chimbuko la vipaji vya michezo.
“Nawashukuru sana waandaaji
wa mbio hizi za Rock City Marathon kwa kuweza kuandaa shindano ambalo
limeweza kutusaidia sisi wadau wa riadha kugundua vipaji vingi ambavyo
tunavyo hapa nchini. Hivi vipaji vinastahili kukuzwa. Hivyo basi natoa
wito kwa watu wote wenye dhamana ya michezo kutumia mbio hizi kama
chambo cha kuweza kutambua vipaji vingi vya riadha ambavyo vinahitaji
kuendelezwa kwa manufaa ya taifa,” alisema Bw Kizito.
Pamoja na hayo mashindano haya yameweza kufanikiwa kwa udhamini wa
makampuni mbalimbali nayapongeza kwa juhudi zao za kuweza kuinua michezo
hapa mkoani Mwanza na Tanzania kwa ujumla. Nayaomba na makampuni
mengine kujitokeza kudhamini michezo hii kwani fursa kwao katika
kutangaza bidhaa zao.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu
wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui alisema Rock
City Marathon imeonyesha kukua kila mwaka, kwa kuwa inauwezo wa
kukimbiza mbio za ngazi zote; nusu marathon, kilometa tano, kilometa
tatu kwa walemavu, kilometa tatu kwa wazee na kilometa mbili kwa watoto.
Alisema Shirikisho
limezingatia usimamizi mzuri wa Rock City Marathon na lipo tayari kutoa
kibali kitachacho iwezesha kampuni ya Capital Plus International kuandaa
mbio ndefu za kilometa 42 (full Marathon) watu wakiweza kuhamasika na
kushiriki kwa wingi.
Washiriki kutoka mikoa mbali mbali waliweza kushiriki na wageni kutoka
nchi kama Kenya and Uganda, India, Canada, Australia, Africa Kusini,
Rwanda, pia walishiriki.
Mbali na medali walizopata washindi hawa, zawadi za fedha taslimu
zilitolewa ambapo washindi wa pili katika mbio za kilometa 21, upande wa
wanaume na wanawake walipata 900,000/- na vingamuzi vya Continental
kila mmoja.
Washindi wa tatu kilometa 21 wakiondoka na kingamuzi na 700,000/- na
decoda za Continental kila mmoja kwa upande wa wanaume na wanawake.
Muhindiro Yusto kutoka Mwanza aliyeshinda kilometa tatu kwa upande wa
wazee na Benard Samike wa Mwanza kwa upande wa watu wenye ulemavu .
Kwa upande wa watoto ambao
walikimbia kilometa mbili, Benedicto Mashauri wa mwanza alishika nafasi
ya kwanza huku Suzana Madary wa Mwanza akingara kwa upande wa wasichana. Picha zote na G sengo Blog
No comments:
Post a Comment