DKT. SHEIN AZINDUA MADARASA YA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 8 September 2013

DKT. SHEIN AZINDUA MADARASA YA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni  Nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,wakikata utepe kama ishara ya ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni  Nje ya Mji wa Unguja.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,Dk.Haji Mwita,alipotembelea kuona vifaa mbali mbali vya kufundishia chuoni hapo alipofika kuzindua madarasa ya kusomea yaliyojenga kwa ufadhili wa Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake,baada ya kuyazindua rasmi madarasa ya chuo hicho leo ,hapo chuoni Mbweni,Mkoa wa Mjini Magharabi  Nje ya Mji wa Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Dk. Haji Mwita,baada ya kuyazindua Rasmi madarasa ya Kusomea, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,akitoa salamu
zake wakati wa sherehe za uzinduzi wa madarasa mapya ya kusomea katika Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya, yaliyojengwa na  Serikali ya Oman,na ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 
Baadhi ya wananchi na viongozi walioalikwa katika sherehe za  uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni  Nje ya Mji wa Unguja leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

No comments:

Post a Comment