Mwenge huo wa Uhuru umetembelea miradi
23 ya maendeleo na miradi 28 ya vikundi Mkoani Rukwa vyenye thamani ya
fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni 3.4 ikiwa ni mchango wa
Serikali kuu, Halmashauri, Wananchi na Wadau wengine wa maendeleo.
Ndege ndogo ya Shirika la hifadhi za
Taifa (TANAPA) ikipaa angani katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga ikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya, wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa sita pamoja na Mwenge wa
Uhuru utakaoenda kukabidhiwa Mkoani Tabora na Mkuu huyo wa Mkoa wa
Rukwa. Wakimbiza mwenge hao ni Ndugu Juma Ali Simai (Kiongozi), Zamda A.
John, Christopher Emmanuel, Seperatus Lubinga, Zuwena Abdallah na Mgeni
S. Mgeni.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew
Sedoyyeka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya
Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukamilisha ratiba yake katika Wilaya hiyo
na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mkuu huyo wa Mkoa atasafiri kwa ndege
kuukabidhi Mwenge huo Mkoani Tabora.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa hotuba ya kuwaaga
wakimbiza mwenge kitaifa na Mwenge wa Uhuru muda mfupi kabla ya kusafiri
na Mwenge huo kwa ajili ya kuukabidhi Mkoani Tabora. Katika hotuba yake hiyo aliwapongeza wakimbiza Mwenge
wote na wananchi Mkoani Rukwa kwa kufanikisha zoezi hilo kikamilifu na
kuwapa vyeti vya pongezi wakimbiza Mwenge hao wa kitaifa.
Picha
ya pamoja kati ya kikundi cha matarumbeta kilichokuwa mstari wa mbele
katika kutumbuiza kwenye ziara ya Mwenge Mkoani Rukwa na baadhi ya
wakimbiza Mwenge kitaifa na mratibu wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu
Abubakari Serungwe wa kwanza kulia (mbele).
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizungumza na wananchi
wa Manispaa ya Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi Mjini Sumbawanga. Kulia ni Diwani wa kata ya katandala Ndugu
Kisabwite na Mbunge Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan
Kmanta akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a Mwenge wa
Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo machachari
katika mbio za mwenge wa Uhuru Moshi Chang'a akimkabidhi Mkuu wa Wilaya
ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza
mbio zake Wilayani Kalambo.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Methwew Sedoyyeka akipokea mwenge wa Uhuru
kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a
na kuahidi kuukimbiza katika wilaya yake kwa amani, nguvu na uadilifu
mkubwa.
Baadhi ya raia wa kigeni nao waliomba kupiga picha na Mwenge wetu wa Uhuru.
Wananchi na wanafunzi walihamasika vya
kutosha na Mwenge wa Uhuru kiasi cha wengine kupanda juu ya miti ili
waweze kupata taswira yake mwanana.
Wanafunzi na wananchi wakiwa juu ya miti kushuhudia Mwenge wa Uhuru na ujumbe wake.
Kwa wengine kuuona Mwenge wa Uhuru vizuri haikuwa kazi rahisi walilazimika hata kuhatarisha maisha yao.
Picha
ya pamoja kati ya mratibu wa Mwenge Mkoani Rukwa ndugu Abubakar
Serungwe na baadhi ya wakimbiza mwenge kitaifa pamoja na katibu wa CCM
Sumbawanga Mjini Mama Silaf Maufi.Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment