Mshiriki mwingine wa shindano la Bibi
Bomba.Bi.Tabitha Tungaraja akishukuru Mungu mara baada ya jina lake
kutajwa na kuingia kwenye ushiriki wa shindano hilo,mbele ya baadhi ya
waratibu wa shindano zima
Pichani wa pili kushoto ni Meneja wa
Clouds TV ambao ndio warushaji wa shindano la Bibi Bomba season
2,Bwa.Lee Ndayisaba akifafanua jambo mbele ya washiriki wa shindano hilo
na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana uendeshaji na mchakato mzima
wa shindano hilo ambalo limekuwa na msisimko mkubwa kwa watazamaji.Shoto
ni mmoja wa waratibu wa shindano hilo Babuu wa Kitaa (Clouds TV),tatu
shoto ni wawakilishi wa shirika la USAID,Bi.Naomi Kaspar pamoja na
Dkt.May Bukuku, ambao wametoa mchango mkubwa kufanikisha maandalizi ya
shindano hilo.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Bibi Bomba awamu ya pili 2013 wakiwa ndani ya ukumbi wa alliance française wakisiliza mchakato mzima wa utaratibu wa shindano hilo.
Baadhi ya Mabibi Bomba wakifurahi jambo.Picha na Michuzijr.Blogspot.com
--
Shindano hilo
lilianza mchakato wake wa usaili katika viwanja vya Leaders Club,
ambapo Mabibi zaidi ya 60 walijitokeza aidha kati yao waliingia katika
mchujo wa awali na kupatikana Mabibi 20 ambao wameendelea kupigiwa kura
hadi hii leo.
Shindano la Bibi
Bomba season 2 limezinduliwa rasmi hapo jana katika ukumbi wa Alliance
Française, ambapo bibi 20 wanaingia rasmi katika kinyanganyiro cha
kumtafuta bibi Bomba kwa mwaka 2013.
"siku zote
panapokuwa na watu wengi lazima vituko, kero ama ubabe lazima vinanafasi
ya kujitokeza ili kutimiza ule msemo wa kiswahili unaosema “penye wengi
kuna mengi” ..tunatarajia msisimko wa aina yake katika mashindano haya
kwa mwaka huu.
tofauti pia na
mwaka jana ambapo shindano hili lilidumu kwa mwezi mmoja,na mwaka huu
Bibi bomba itachukua takriban miezi 3.Mengi mtayapata wakati kipindi
kikiwa kinaruka kuanzia saa mbili na nusu usiku",alimaliza kusema Lee wa
Clouds TV ,kituo ambacho kitakuwa kikirusha shindano hilo.
No comments:
Post a Comment