Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Mh. Godbless Lema akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho kuwania Udiwani wa Kata ya Kaloleni, mkutano uliofanyika eneo la Ekenya studio (mashariki ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid) . Katika Mkutano huo Lema aliainisha ufisadi mkubwa wa jumla ya sh. 12 bilioni uliofanywa na watumishi wa Halamshauri ya Manispaa ya Arusha akirejea taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka unaoishia 2012, ikiwemo kutowasilishwa kwa makusanyo ya ushuru mbalimbali na matumizi mengine kukosa nyaraka za kuthibitisha matumizi yake.
Umati wa wananchi na baadhi ya viongozi katika mkutano huo
Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini, Martin Sarungi (kulia) akiwa na Mgombea wa Chadema Kata ya Themi, “Kabouru” (katikati) katika mkutano wa Kampeni eneo la Relini.
Diwani wa Chadema Halmashauri ya Moshi, Mh. Hawa Ali
Kiongozi wa Vijana wa Chadema Korogwe na Mjumbe wa Baraza la Kanda ya Kaskazini Chadema, Bi Aminata .
Huyu ni Annarose, mwana mama ambaye ana nia ya kuwania Ubunge mwaka 2015 katika Jimbo analoongoza Mh. Lyatonga Mrema (TLP) kwa sasa.
Kiongozi wa Vijana Chadema Wilaya ya Hai, Mss Doris Cornel akifafanua jambo mkutanoni hapo
Diwani wa Kata ya daraja Mbili, Mh. Msofe nae alikuwepo mkutanoni hapo kumnadi mgombea wa Chadema
Mjumbe wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Usa River, Arumeru Mashariki Mh Josephine Annaely akisisitizia umuhimu wa wananchi kutumia fursa ya kupiga kura
Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA WIlaya ya Arusha Mjini, Noel Ole Varoya akihutubia. Noel alitumia nafasi hiyo kukemea vikali vitendo vya baadhi ya wanasiasa wanaohubiri udini na ukabila kwa nia ya kuwagawa watanzania ili wawatawale ama wapate manufaa yao kisiasa, na kudai kwamba hali hiyo ikiachwa iendelee italeta kadhia ambayo hakuna mtu atakayekuwa salama na watanzania hawataulizia tena dhahabu na mali zao viko wapi.
Mgombe mwenyewe wa Udiwani Kata ya Themi kupitia Chadema kimwaga sera zake
Boss mzito wa Arusha255 akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani na vicheko vya hapa na pale mkutanoni hapo
No comments:
Post a Comment