GIDABUDAY AMTUMIA MWANAE JEZI YA TANZANIA ILI KUITANGAZA NCHI TANZANIA KATIKA MBIO HUKO BRONCO CALIFORNIA-MAREKANI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Jun 2013

GIDABUDAY AMTUMIA MWANAE JEZI YA TANZANIA ILI KUITANGAZA NCHI TANZANIA KATIKA MBIO HUKO BRONCO CALIFORNIA-MAREKANI


Pichani ni jezi ya Tanzania atakayotumia Sydney Gidabuday katika mashindano ya mbio huko Calfornia.
Sydney Wilhelm Gidabuday ni mwanariadha wa kimarekani mwenye asili ya kitanzania na mtoto wa mwanariadha wa zamani  na mwanaharakati wa michezo nchini,na  aliwahivunja rekodi miaka ya 1994 nchini Marekani ambaye jina lake si geni masikioni mwa watanzania "Wilhelm Gidabuday".
Japokuwa Sydney ni mmarekani mwenye mapenzi na uzalendo wa kuitangaza nchi ya baba yake Gidabuday yaani "Tanzania", tayari amekwisha pokea jezi  atakayotinga katika mashindano ya riadha ya BRONCO INVITATION JUNE 22, CALIFORNIA MAREKANI. Jezi ya Tanzania iliyotumwa kutoka Tanzania na wanariadha wa kitanzania yani "Phaustin Baha na Wilhelm Gidabuday, tayari imekwishafika katika mikono ya Sydney huku akiahidi kuitendea haki katika mashindano hayo.

Sydney Wilhelm Gidabuday
MAONI KWA SERIKALI.
Kuwa na uraia wa nchi mbili sio sababu ya kutoipenda Tanzania yetu, bali ni njia muafaka ya kuifungua milango na mianya ya kuleta mafanikio na kulitangaza taifa letu la Tanzania katika nchi mbali mbali duniani.

WITO KWA SERIKALI KUTOKA KWA GIDABUDAY - BABA YAKE "SYDNEY - GIDABUDAY".
"Mimi baba yake, naliomba bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhalalisha SHERIA YA URAIA WA NCHI MBILI ili mtoto wangu "Sydney" aweze kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Riadha kitaifa na kimataifa, kwani ana uzalendo sana na nchi hii ya Tanzania japokuwa yeye ni Mmarekani",uzuri shule ya msingi alisoma Arusha Tanzania".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad