Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mwamini Malemi akimsalimia Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu
ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta (Kulia) wakati alipokuwa anawasili
katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro kwa ajili ya kufunga
rasmi mafunzo ya Jinsia kwa maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza.
Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma
Malewa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mwamini Malemi akizungumza na maafisa mbalimbali wa Jeshi la
Magereza kabla ya kufunga mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Malemi
licha ya kulipongeza jeshi hilo kwa hatua nzuri ya kuwateua maafisa
mbalimbali wanawake, alilitaka jeshi hilo kuongeza juhudi zaidi kwa
kuwapa nafasi ya uongozi wanawake ambao wana uwezo na sifa ya kuongoza.
Maafisa Magereza wakiifurahia hotuba ya mgeni rasmi,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
alipokuwa anatoa hotuba ya kufunga mafunzo ya jinsia yaliyokuwa yanafanyika
mjini Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Mwamini Malemi (Kulia), akipokea
taarifa ya hali ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika Taasisi
zinazotekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kutoka kwa Mshauri
wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini,
Bi. Wanyenda Kutta . Kushoto ni Dk Juma Malewa, Kamishna wa Sheria na
Utawala wa Jeshi la Magereza
Naibu Katibu Mkuu Mwamini Malemi (wa pili kutoka
kulia) akimpa zawadi askari wa Jeshi la Magereza kutoka Gereza la Wilaya
ya Liwale, mkoani Lindi, Beatrice Sabo kwa kuwasilisha vizuri mada ya
jinsi na jinsia wakati wa mafunzo hayo. Wa kwanza kutoka kushoto ni
Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa.
Anayefuata ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko
ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta. Kulia ni Mwezeshaji wa
mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Asina Omari.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment