MUONEKANO: MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA KUZALIWA KWA CCM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday 6 February 2013

MUONEKANO: MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA KUZALIWA KWA CCM

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa hotuba yake kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Mkoani Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisema machache,muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani} kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma.
Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma na kuwahakikishia kuwa sasa hivi mkoa wa Kigoma mambo yako vyema kabisa na treni itaendelea kufanyaka kazi kama zamani.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akiongoza shughuli hiyo.
 Ankal Issa Michuzi (wa pili kulia) akiwa na wanahabari wa Kigoma.
 Wanahabari waliorekodi sherehe hizo kutoka vyombo mbalimbali.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia burudani ya ngoma. 
Chipukizi wa CCM Mkoa wa Kigoma wakifanya Gwaride la heshima kwa Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM,yaliyofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

 Mtangazaji mkongwe wa TBC Taifa Swedi Mwinyi akiwa hai hewani na wenzie
 Katibu Mkuu wa CCM akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Omar Chambo na Maafisa waandamizi wa wakala wa usafiri wa anga.
 Washindi wa kombe la CCM 2013
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea banda la Uhuru na Mzalendo
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mang'ula akipitia magazeti ya zamani kwenye banda la Uhuru na Mzalendo
 Ngoma toka mkoa wa Makamba nchini Burundi
 
Mablogger wakirekebisha mitambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia. Kutoka kushoto ni Ahmad, Othman, Bukuku, Nkoromo na Mroki.

No comments:

Post a Comment