Wataalamu
wa ujenzi pamoja na wawakilishi wa Shirika la NSSF katika picha ya
pamoja mara baada ya makabidhiano ya Jengo kubwa na la kisasa la shirika
hilo lililojengwa Jijini Arusha, barabara ya Old Moshi. Jengo hilo
lenye jumla ya ghorofa 15, mbili zikiwa chini (basement) kwa ajili ya
maegesho ya magari linaelezwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 28.75
na limejengwa kwa muda wa miaka miwili.
Kamapuni ya China
Jiangchang Engineering Co. Ltd (CRJE) ndiyo imekabidhi mradi huo ramsi
hii leo baada ya kukamilika ujenzi wake uliowashirikisha pia wakandarasi
wadogo 6 wa ndani.
Jiji la Arusha limepata muonekano mpya kwa
kuongezewa jengo refu, kubwa na la kisasa kwa shughuli za kiosifi na
biashara. NSSF nao wanategemea kuhamishia offisi zao kwa kanda hii
katika jengo hili, halikadhalika huduma za kibenki zitapatikana hapo.
Sehemu ya mbele ya jengo, upande wa kushoto
Jengo
jipya la Shirika la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililoko Jijini
Arusha, Barabara ya Old Moshi. Jengo hilo limekabidhiwa leo kwa shirika
hilo toka kwa mkandarasi kutoka China ambae alishirikiana na wakandarasi
wengine wa ndani.
Mkadiriaji
na msimamizi wa gaharama za mradi, QS Komba akifafanua jambo kwa
mwakilishi wa NSSF, Eng. Mattaka wakati wa ukaguzi wa jengo hilo leo
kabla ya makabidhiano ramsi.
Timu ikifanya ukaguzi eneo la kuegesha magari ndani ya jengo hilo.
Mbunifu
wa jengo, mwakilishi wa NSSF, Injinia Mshauri pamoja na injinia mkaazi
wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa maalumu kwa ajili yao na
wataalalmu wengine walioshiriki katika ujenzi wa mradi huo, katika
hoteli ya kitalii ya Kibo Palace ya Jijini Arusha.
Wakandarasi wa kichina pamoja na mkadiriaji majengo wa mradi, QS Komba wakiwa katika maankuli.
Mkadiriaji
majenzi wa mradi huo, QS Komba na wataalamu wengine waliofanikisha
mradi huo, pamoja na mwakilishi wa NSSF wakiangalia picha za jengo hilo
walizopiga hii leo Jijini Arusha.
Architect
Dudley Mawalla kutoka MD Consultancy Ltd ya Jijini Dar es Salaam
(aliyekunja mikono), ambae ndiye mbunifu wa jengo hilo la NSSF Jijini
Arusha katika mkutano wa makabidhiano ya mradi baada ya kukamilika kwa
matumizi hii leo.
Wataalamu
walifanikisha design na michoro ya jengo hilo, wakandarasi wa kichina
pamoja na mwakilishi wa NSSF, Eng Mataaka wakibadilishana mawazo mara
baada ya kikao cha makabidhiano ya mradi kutoka kwa mkandarasi kwenda
kwa NSSF.
Injinia
Mattaka (katikati) kutoka NSSF akipata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu
wa usalama wa jengo hilo namna ambavyo mitambo ya kiusalama imefungwa na
inavyofanya kazi.
No comments:
Post a Comment