MFANYABIASHARA wa madini aina ya Tanzanite mkoani Arusha,Ngerii Olerumwa anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 amekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha ndani ya hoteli ya Premier Palace ambayo timu ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano imeweka kambi hotelini hapo jijini Arusha.
Maiti ya mfanyabiashara huyo
iligundulika majira ya saa 3 ;30 asubuhi leo mara baada ya mhudumu wa
hoteli hiyo kugonga kwa muda mrefu mlango wa chumba alichokuwa amefikia
marehemu huyo bila mafanikio na kisha kubaini alikuwa amefariki dunia.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo akiwemo meneja wa hoteli hiyo ambaye alikataa kutaja jina
lake hadharani alisema kwamba marehemu huyo aliwasili hotelini hapo
mnamo desemba 3 mwaka huu majira ya saa 1 ;00 jioni na kukodi chumba
kimojawapo hotelini hapo.
Meneja huyo akisimulia tukio
hilo alisema kwamba marehemu aliwasili akiwa peke yake hotelini hapo na
kubainisha kwamba yeye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kukodi chumba
hotelini hapo.
Hatahivyo,alidai kwamba
ilipotimu leo majira ya saa 3 ;30 asubuhi wakati mhudumu wa hoteli hiyo
akigonga mlango wa chumba alichofia marehemu kwa lengo la kufanya usafi
mlango huo haukuweza kufunguliwa kwa wakati hali iliyowapelekea kufanya
juhudi za kuufungua mlango huo kwa lazima.
Alisema kwamba baada ya
kufanikiwa kuufungua mlango huo walijaribu kumwamsha marehemu lakini
hakuweza kuamka hali iliyowapelekea kuliarifu jeshi la polisi kuhusiana
na tukio hilo.
jamii blog lilipofika
maeneo ya hoteli hiyo liliwashuhudia askari wa upepelezi kutoka jeshi la
polisi mkoani hapa wakichukua maelezo kwa baadhi ya watumishi wa hoteli
hiyo wakiwemo walinzi wa hoteli hiyo huku baadhi ya wabunge wanaounda
timu ya wabunge wa bunge la jamhuri wakitaharuki kutokana na tukio hilo.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti ndugu wa marehemu ambao walikusanyanya nje ya hoteli hiyo
walisema kwamba wameshtushwa na kifo cha ndugu yao na wanahisi kwamba
aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha huku wakilitaka jeshi la polisi
kubaini chanzo cha kifo cha marehemu.
Akihojiwa na waandishi wa
habari kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas
alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kwamba jeshi lake
linachunguza kwa kina kifo hicho.
Sabas,alisema kwamba mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya
hospitali ya mkoa ya Mt,Meru na atatoa taarifa kamili ya tukio hilo
kuanzia leo mbele ya waandishi wa habari. Na pamela Mollel
No comments:
Post a Comment