Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati alipofungua rasmi Jengo
la Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Kinyonga,wilayani Kilwa jana
wakati wa kilele cha ziara yake ya siku tano ya kikazi Mkoani
Lindi.Kulia aliyesimama ni Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dkt.Mike
Mabimbi.
Mganga mkuu katika hospitali ya
Kinyonga,wilayani Kilwa Dkt.Mike Mabimbi(kulia) akitoa maelezo kwa Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kufungua jengo la
wazazi katika hospitali hiyo na kulikagua.Wodi hiyo ya Wazazi imejengwa
ikiwa ni Mkakati wa kuboresha huduma ya Mama na mtoto Tanzania na ujenzi
umefadhiliwa na Halmashauri ya Kilwa pamoja na Chama Cha Madaktari
Bingwa wa Magonjwa ya akina mama Tanzania(AGOTA) na shirika la Uholanzi
la Bioshape Benefit Foundation.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiwahutubia wananchi mjni Kilwa Kivinje jana jioni.Rais Kikwete
aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi amerejea
jijini Dar es Salaam jioni hii.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akingalia wanafunzi wakifanya majaribio ya kisayansi katika shule ya
sekondari ya Mitole iliyopo wilayani Kilwa, wakati alipokuwa katika
ziara ya kikazi Mkoani Lindi jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara
mjni Kilwa Kivinje,mkoani Lindi jana jioni.Picha na Freddy Maro-IKULU
No comments:
Post a Comment