Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Clouds
Media Group,Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake,akiwemo mwanamuziki
nyota wa dansi ndani ya kundi la Wenge BCBG,kutoka nchini DRC-Congo,JB
Mpiana (pichani kati) kwenye hafla fupi ya chakula cha usiku
iliyofanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape 2,kilichopo Kunduchi
jijini Dar,hafla hiyo pia ni sehemu ya muendelezo wa shamra shamra za
maadhimisho ya miaka 13 ya Clouds FM tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph
Kusaga akiwakaribisha wageni wake na kuzungumza nao machache na
kuhakikisha wanapatiwa chochote kitu.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph
Kusaga akimtambulisha mke wake Johayna Kusaga (ambaye ndiye Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Prime Time Promotions Ltd) kwa Mwanamuzik JB
Mpiana na kwa wageni wengine waliofika kwenye hafla hiyo ya chakula cha
pamoja.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake JB Mpiana kwenye chakula
Pichani ni baadhi ya Washiriki wa
shindano la Miss East Afrika 2012 ambao pia waliakwa kwenye chakula cha
pamoja ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2,kilichopo Kunduchi jijini
dar.
Washiriki wa shindano la Miss East Afrika wakiwa katika picha ya pamoja
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Cassim akitumbuiza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali
Boniventure Kilosa a.k.a Dj Venture
alikamata mashine na kuangusha ngoma kali zikiwemo za Kinaija,abazo
wageni wengi walionekana kuburudishwa nazo vilivyo.
Washiriki wa shindano la Miss East Afrika 2012 wakijiachia vilivyo kwa mikato ya ngoma iliokuwa ikiangushwa na Dj Venture.
Joseph Kusaga a.k.a Boss Joe
akizungumza na baadhi ya wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ay na
Mwana FA ndani ya hafla fupi ya chakula cha usiku kulichoandaliwa kwa
ajili ya wageni.
Wadau nao walikuwepo.Mdau wa MJ FM pamoja na Andrew Kusaga wakishoo love.
Wafanyakazi mbalimbali kutoka Clouds Media Group walikuwepo pia |
Mtangazaji wa Clouds TV,Ben Kinyaiya kifanya mahojiano mafupi na mwanamuziki mkongwe wa dansi,Ndandaa Kossovo.
Dj Venture na mshkaji wake wakivuta pumzi.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time
promotios,pichani kulia Godfrey Kusaga akibadilishana mawazo na
Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM,Ephrahim Kibonde
huku wakiangusha moja moja.
Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo.
No comments:
Post a Comment