NDEGE INSURANCE BROKERS YAZINDUA NEMBO MPYA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 22 November 2012

NDEGE INSURANCE BROKERS YAZINDUA NEMBO MPYA



Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege akimkabidhi Mgeni rasmi Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora tuzo ya heshima kubwa kwa kutoa mchango mkubwa  kwa namna moja ama nyingine katika kampuni hiyo ya Ndege Insurance,hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya hotel ya Serena,jijini Dar.
Mfanyakazi Bora wa Mwaka wa kampuni ya Ndege Insurance Brokers Bw. Haruna Said akikabidhiwa tuzo yake na Mgeni rasmi Bw. Israel Kamuzor.
Mwanasheria wa kampuni ya Ndege Insurance Brokers Bw. Justin Ndege akikabidhi tuzo kwa mfanyakazi aliyedumu muda mrefu katika kampuni hiyo Bi. Eutrophia Benedict (kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni mgeni rasmi na Dkt. Sebastian Ndege.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 45 tangu kuanzishwa kwake ikiwemo sambamba na kuzindua nembo yake mpya ya Ndege Insurance Brokers.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Renatha Mushi akimlisha keki Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Renatha Mushi akiandaa keki ya kulimsha Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege
Mgeni rasmi Bw. Israel Kamuzora (katikati) wakikata keki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege (kulia) pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Bi. Renatha Mushi Ndege ikiwa ni maaadhimisho ya miaka 45 ya tangu kuanzishwa kwake kutoa Huduma za Bima nchini.
Makofi baada ya keki kukatwa



Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Bw. Israel Kamuzora akizindua nembo mpya ya Ndege Insurance Brokers kwenye hafla ya kutimiza miaka 45 ya kampuni hiyo. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Dkt. Sebastian Ndege.
 SKYLIGHT BAND ikota burudani kusindikiza maadhimisho ya miaka 45 ya Ndege Insurance Brokers tangu kuanzishwa kwake.
Wanahabari wakiwa bize kuchukua tukio la kukatwa kwa keki

Mmoja wa waimbaji wa bendi ya Skylight akiimba jukwaani wakati wa hiyo ilipokuwa ikiendelea.
Wadau Bukuku, Kibonde waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
Wadau mbalimbali wakishuhudia tukio adhimu la mafanikio makubwa ya Ndege Insurance Brokers .
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Ndege Dkt. Sebastian Ndege akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 45 ya Kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake, iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya  Serena jijini Dar es Salaam.

1 comment: