Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani, kupitia Wakili wao Alute Mughwai ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe, limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu
kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku
14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za walio kata rufaa.
Mawakili wa Mh Godbless Lema wanahitajika kutimiza majalada ya kisheria ndani ya siku 14 ili shauri la rufaa hiyo iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa na kuamuliwa.
Wadaiwa kwenye
shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa
Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua
ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa
CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matu
Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Tindu Lissu.
Baadhi ya wananchi, wapenzi wa Chadema wakimlaki Mh. Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama.
Kutoka kushoto, Henry Kileo, Nuru Ndosi na Mh. Godbless Lema.
Henry Kileo akiwa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam
Katibu
wa Chadema Kanda ya Kinondoni, Henry Kileo (kushoto) akibadilishana
mawazo na mdau wa Chadema mara baada ya kuwasili viwanja vya Mahakama
Kuu. Kwa hisani ya Arusha255.blogspot.com
No comments:
Post a Comment