WAZIRI MKUU MSTAAFU AWAASA WAREMBO WA MISS TANZANIA KUTUMIA FANI ZAO KAMA AJIRA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 10 October 2012

WAZIRI MKUU MSTAAFU AWAASA WAREMBO WA MISS TANZANIA KUTUMIA FANI ZAO KAMA AJIRA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akisalimiana na Mrembo wa mkoa wa Rukwa ambaye anaiwakilisha kanda ya Kaskazini, Vency Edward. Warembo wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012  walimtembelea nyumbani kwake eneo la Ngarash mjini Monduli, mkoani Arusha.












WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa amewataka warembo wanaoshiriki mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2012 kutumia nafasi hiyo waliyopata kutengeneza ajira kwao na vijana wenzao.



Lowasa ameyasema leo wakati warembo wanaowania taji hilo walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Ngarash mjini Monduli na kuzungumza nao juu ya mambo mbalimbali ya kisiasa, uchumi, utalii na sanaa ya urembo.



“ninyi ni vijana, mnanguvu na hakika mkiyatumia vyema mashindano haya kwa malemngo yanayostahili mnaweza kufika mbali kimaisha kwa kuwa wabunifu wa vitu mbalimbali vya kufanya katika jamii na kujipatia ajira yenu binafsi na hata kuajiri watu wengine,”alisema Lowasa.

Na Father Kidevu Blog ( www.mrokim.blogspot.com) , Ngarash-Monduli

No comments:

Post a Comment