Makamu
wa Rais wa chama cha wafanyabiashara wa Uingizaji na Usafirishaji wa
dawa na vifaa tiba kutoka China (CCCMHPIE) Meng Dongping akizungumza
Sept 18,2012 katika mkutano wa wafanyabiashara wa Uingizaji na
Usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka nchini China amesema Tanzania ni nchi
ya 11 katika ushirikiano wa kibiashara wa bidhaa hizo barani Afrika na
nchi ya pili kwenye soko la bidhaa hizo wa nchi za EAC. ambapo katika
kipindi cha miezi 6 cha mwaka 2012 ukuaji wa soko la bidhaa hizo nchini
Tanzania umefikia dola za Marekani milioni 32.61 sawa na asilimia 47 .
Makamu
wa Rais wa chama cha Wafanyabiashara wa Uingizaji na Usafirishaji wa
dawa na vifaa tiba kutoka China (CCCMHPIE) Meng Dongping (kulia)
akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na
Dawa nchini (TDFA) Haiiti Sillo katika mkutano huo wa siku moja jijini
Dar- es -Salaam .
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbalizilizotolewa na watoa mada wa mkutano huo.
Washiriki wa mkutano huo kutoka China na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.
(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO) .
No comments:
Post a Comment