Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto
Agnes Wanjiru, 5, wakati alipowasiri kwenye kituo cha kulelea watoto
wadogo cha Thomas Barnados mjini Nairobi.
Jamani haka katoto kazuri..!!! |
Mama
Salma Kikwete akiwa katika kituo cha kulelea watoto wadogo cha Thomas
Barnados aliweza kuwapakata, kuwabeba watoto mbalimbali wanaolelewa
kituoni hapo.
Mama
Salma Kikwete akiangalia kazi za wanafunzi wa chekechea wanaolelewa
katika kituo cha Thomas Barnados kilichopo jijini Nairobi wakati
alipotembelea shuleni hapo. Mama Salma ameambatana na
Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Kenya.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa
mwanafunzi wa 'Starehe Girls Centre' waliokuwa katika maabara ya shule
hiyo wakifanya practicals katika somo la kemia. Shule hiyo huchkua
watoto wanafanya vizuri katika masomo ya msingi lakini hukosa uwezo wa
kujiunga na sekondari.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali za ufinyanzi
zinazotengenezwa na kiwanda cha Kazuri kilichoko Nairobi.Picha na John Lukuwi
No comments:
Post a Comment