Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi katoni ya chumvi Mtoto mwenye ulemavu wa kutokuona Husna Rajabu, kwa niaba ya watoto wenzake ambao ni walemavu wasiona na wanaoona wa shule ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,alieshikilia mbuzi kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi mbuzi wawili Bi.Rafael Mohamed kwa niaba ya wakina mama wenzake ambao ni walemavu wasioona wa kijiji cha Mnamba kata ya Nyangao Mkoani Lindi,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali inayoendeshwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,anaeshuhudia wapili toka kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon.
.Baadhi ya watoto wa shule ya Msingi ya Nyangao iliyopo Lindi Vijijini wakiwa wamebeba mfuko wa sembe mara baada ya kukabidhiwa msaada huo na Mkuu wa Kitengo cha odacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule hayupo pichani ikiwa ni mwendelezo wa kutoa misaada na kufuturisha watoto yatima na wasiona katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa kupitia kampeni ya Ramadhan Care and Share wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
No comments:
Post a Comment