Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima
Dendego pichani kati mwenye kipaza sauti akisoma namba za washindi
waliojinyakulia piki piki mbili zilizotolewa na kampuni ya Push Mobile,
wa tatu kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rugambo Rodney
na mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media
Group,Joseph Kusaga,na nyuma kabisa ni Mkurugenzi wa utafiti Clouds
Media Group, Ruge Mutahaba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya
bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru wakishuhudia tukio hilo usiku huu
kwenye uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012
linafanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima
Dendego akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media
Group, Joseph Kusaga usiku huu mara baada ya kuwataja washindi
waliojishindia piki piki mara baada ya kuchezeshwa bahati nasibu,wakati
tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea,pichani kati ni Afisa
Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
Nuru akitumbuiza jukwaani usiku huu na shabiki wake mbele ya wakazi wa
jiji la Tanga wanaondelea kutiririka ndani ya uwanja wa Mkwakwani
ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Rachel wa THT,akifanya vitu vyake kwenye jukwaa la Fiesta Tanga.
Pichani shoto ni Mkurugenzi wa
Masoko, Ephrahim Mafuru, Mkuu wa Vipindi Clouds FM,Sebastian Maganga
sambamba na Meneja wa bia ya Serengeti,Allan Chonjo wakiwa katika picha
ya pamoja ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati tamasha la Serengeti
Fiesta likiendelea kurindima.
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Tanga wakifuatilia kwa makini makamuzi ya Fiesta 2012
No comments:
Post a Comment