Mwandishi Mkongwe hapa nchini,Mzee Fili
Karashani ambaye aliwahi kupata tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika
Tasnia ya Habari mwaka 2011,katika tuzo ya Wanahabari Bora wa Mwaka
2011,akifafanua jambo kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa
vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya
iliyowahusu Wanahabari/Wachora Katuni na wadau wengine mbalimbali
iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark hotel,Ubungo jijini Dar
Es Salaam.Semina hiyo imeandaliwa na Kikundi Cha Sheria na Haki za
Binadamu Cha TIFPA kwa Msaada wa Shirika la Ford Foundation la Marekani .
Baadhi ya Wanahabari,Wachora Katuni na
Wadau wengine mbalimbali wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa
zikitolewa kwenye semina elekezi ya jinsi ya ushiriki wa vyombo vya
habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya iliyofanyika
kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark hotel,Ubungo jijini Dar Es
Salaam.Semina hiyo imeandaliwa na Kikundi Cha Sheria na Haki za Binadamu
Cha TIFPA kwa Msaada wa Shirika la Ford Foundation la Marekani .hiyo
kuhusiana na mchakato wa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya na pia namna ya
kuielimisha jamii katika umuhimu wa kushiriki
Mchora Katuni mahiri Masoud Kipanya na
Mmoja wa watangazaji wa kutoka Times FM Radio Ibrahim Issa wakifuatilia
mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye semina elekezi ya jinsi
ya ushiriki wa vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya
Katiba Mpya iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Land Mark
hotel,Ubungo jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment