Hili nalo neno: Wazee wa Maumau wawasilisha kesi London - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Jul 2012

Hili nalo neno: Wazee wa Maumau wawasilisha kesi London


Wazee wa Maumau
hawa ni wazee wawakilishi wa kundi la mau mau
Kundi la wazee kutoka nchini Kenya wanaodai kuwa walinyanyaswa na kuteswa na utawala wa kikoloni wa Uingereza takriban miaka hamsini iliyopita wamewasilisha kesi yao mjini London.
Mwaka mmoja uliopita Mahakama iliamuru kuwa Serikali ya Uingereza haiwezi kujibu tuhuma za vitendo vya watumishi wa Mamlaka ya ukoloni.
Wapiganaji hao ambao wanadai kunyanyaswa na serikali ya kikoloni wakati wakipigania uhuru wa Kenya kutoka kwa Uingereza.
Wazee hao walikuwa wapiganaji wa kundi la Maumau ambalo lilishiriki harakati za uhuru wa Kenya zaidi ya miaka hamsini iliyopita wanasema waliteswa.

Maumau wafungwa wakisafirishwa

Wanadai kuwa maafisa wa Kikoloni wa Uingereza waliwatendea vitendo vya kinyama ikiwemo kuzuiliwa katika kambi,kupigwa,kudhalilishwa kijinsia na hata baadhi ya wanaume kufinywa sehemu zao za siri.
Yote hayo wanasema ni kwa sababu walipinga utawala wa kikoloni.
Sasa wanataka serikali ya Uingereza iwalipe fidia kutokana na mateso hayo. Mawakili wanaowakilisha kundi hilo wanasema wateja wao ni sehemu ndogo ya mamia ya washiriki walio hai kwa sasa nchini Kenya ambao walipitia mateso kama hayo. Wenzao wengine walifariki katika miaka iliyopita.

Kambi ya wafungwa 1952

Awali serikali ya Uingereza ilikuwa imesema haiwezi kuchukua lawama kwa vitendo vilivyotendwa na a utawala wa kikoloni kati ya mwaka 1950 na 1960.
Hata hivyo mwaka jana Jaji wa mahakama kuu mjini London akatoa uamuzi kuwa kesi ya wapiganaji hao wa zamani ina msingi na inapaswa kusikilizwa.
Sasa wapiganaji hao watapata fursa ya kutoa ushahidi wao mahakamani kupitia wenzao Ndiku Mutua, Paulo Nzili, Wambugu wa Nyingi na mwanamke pekee Jane Mara wote ambao wamefika hapa London kwa shughuli hiyo.
Serikali ya Kenya imeahidi kulipa gharama ya kuendesha Kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad