Dr. Jakaya Kikwete awafariji waliopatwa na msiba kwa ajali ya Meli ya MV Skagit - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Jul 2012

Dr. Jakaya Kikwete awafariji waliopatwa na msiba kwa ajali ya Meli ya MV Skagit

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
 Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi.
  Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali.
Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad