RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA HOSTEL BAGAMOYO, AOMBOLEZA KIFO CHA MAMA MZAZI WA WAZIRI STEPHEN WASSIRA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 29 June 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA HOSTEL BAGAMOYO, AOMBOLEZA KIFO CHA MAMA MZAZI WA WAZIRI STEPHEN WASSIRA



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wenyeji wake  kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris aliyoizindua leo Juni 29. 2012 huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kama Mgeni Rasmi  kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris leo huko Bagamoyo, Mkoa
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wa Marian Girls Secondary school kwenye kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris aliyoizindua huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa shangwe alipowasili katika ukumbi wa mikutano kwenye sherehe za "Holy Ghost Congregation 20th General Chapter katika hosteli ya Misheni ya Kikatoliki ya Stella Maris leo huko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mama wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira (kushoto) , Marehemu Esther Mgaya Mankaba, leo nyumbani kwa Mhe Wassira jijini Dar es salaam. Baada ya heshima za mwisho mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea wilayani Bunda kwa mazishi.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCMNape Nnauye, na wanafamilia wa wafiwa  wakitoa heshima za mwisho kwa mama wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira (kushoto) , Marehemu Esther Mgaya Mankaba, leo nyumbani kwa Mhe Wassira jijini Dar es salaam leo. Baada ya heshima za mwisho mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea wilayani Bunda kwa mazishi.
Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment