GREEN WASTE PRO LTD YAKUSUDIA KUIFANYA ILALA KUWA YA KWANZA KWA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 29 June 2012

GREEN WASTE PRO LTD YAKUSUDIA KUIFANYA ILALA KUWA YA KWANZA KWA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM



 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akiwakaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiq (katikati) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala JerrySlaa (wa pili kulia) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar ambapo kampuni hiyo ambayo imeshinda zabuni ya kufanya usafi katika Manispaa ya Ilala.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiq akizungumza na vyombo vya habari ambapo ameipongeza Manispaa ya Ilala kwa kufanikiwa kuingia mkataba na kampuni hiyo wa kufanya usafi katika kata tatu za Manispaa hiyo kwa kuwa Green Waste Pro Ltd ina vifaa na magari ya kisasa, ambayo anaamini yatafanikisha lengo la kuweka jiji kuwa safi.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo  amesema wamekuja viwanja vya Mnazi Mmoja kuonyesha magari waliyonayo likiwemo gari la kisasa la kusafisha barabara, kunyonya mchanga na hata kusafisha barabara kwa maji.

Amesema lengo la kampuni yao ni kuhakikisha Manispaa ya Ilala inakuwa safi akiamini kuwa baada ya miezi michache wananchi wataanza kuona utofauti.
Amefafanua kuwa kwa sasa kampuni ya Green Waste Pro Ltd itaanza kazi ya usafi katika kata za Kivukoni, Mchafukoge na Kisutu.
 
Afisa usafishaji wa Manispaa ya Ilala Samweli Bubegwa (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (katikati) jinsi Manispaa hiyo ilivyodhamiria kufanya usafi na kuwa mfano wa kuigwa miongoni mwa wilaya za mkoa huu na jinsi kampuni ya Green West Pro. Ltd ilivyoweza kushinda Zabuni ya kufanya usafi katika Manispaa ya Ilala.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiq akikata utepe kuzindua rasmi kampuni ya Green West Pro Ltd ambayo imedhamiria kutakatisha Manispaa ya Ilala kwa kuwa ndio kitovu cha jiji la Dar es Salaam. Anyeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (kushoto).
 
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Afisa Usafishaji Manispaa ya Ilala na Mkurugenzi Mkuu wa Green Waste Pro Ltd wakishauriana jambo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akitazama gari la kisasa la kampuni ya Green Waste Pro Ltd lenye uwezo wa kusafisha na kufagia barabara mpaka sehemu za watembea kwa miguu, kunyonya mchanga na pia kusafisha barabara kwa kutumia maji ambalo ni la kwanza na aina yake Afrika Mashariki.
Pichani Juu na Chini ni Muonekano wa magari yatakayotumika katika kampeni ya kusafisha kata tatu za Manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd.
Bw. Sadiq akitazama moja ya Bajaji zitakazotumiwa na kampuni hiyo kuzoa taka katika maeneo ya pembezoni ambapo magari makubwa hayawezi kufika.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kukaguaa vifaa na magari ya kisasa ya kufanya usafi ya Kmapuni ya Green Waste Pro Ltd. iliyoshinda Zabbuni ya kufanya usafi katika Manispaa ya Ilala. Katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd Bw. Anthony Mark Shayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw. Jerry Slaa naye alishiriki kuweka saini katika kitabu hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo.
Meneja Fedha Hillary John Aridai (kushoto) na Meneja Uhusiano Vidah Fammie Joseph wa Kampuni wa Green Waste Pro Ltd pamoja na baadhi ya madereva kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment